Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, kwa mnasaba wa kuhuisha kumbukumbu ya Ashura ya Imam Hussein (as), Ahlul-Bayt (as) na masahaba wao waaminifu, Hizbullah imefanya majlisi za maombolezo ya Muharram katika maeneo ya Hayy al-Sullam, Tahwitat al-Ghadir, Mujtamaa al-Qa'im (aj) katika eneo la Hayy al-Abyadh, pamoja na katika uwanja wa Darat Kayfoun.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na kundi la wanazuoni wa dini, wanaharakati wa kijamii, watu mashuhuri, familia za mashahidi, pamoja na umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kushiriki katika maombolezo hayo ya kumbukumbu ya Karbala na shahada ya Imam Hussein (as).

Maoni yako